The House of Favourite Newspapers

Lucy Komba Arudi Shule

Lucy Komba

STAA wa filamu za Kibongo ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Denmark, Lucy Komba amefunguka kuwa ameamua kurudi shule ili kupata utaalamu zaidi wa masuala ya filamu.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Lucy alisema ameamua kuanza upya kozi ya masuala ya filamu ambayo itamchukua miaka mitatu hivyo akimaliza ndiyo ataanza kufikiria suala la kumzalia mumewe ambaye ni raia wa nchini Denmark, Janus Stanley Landrock.

 

“Huku nimeanza shule upya na ninasoma masuala ya filamu licha ya kwamba nyumbani Bongo zimeshuka naamini kuna siku zitasimama tena au ikishindikana ujuzi wangu nitakaopata nitaenda kuufanyia kazi nje ya Bongo, kuhusu kuzaa kama umri utaruhusu nitazaa nikimaliza kusoma,” alisema Lucy.

STORI: Gladness Mallya

Comments are closed.