The House of Favourite Newspapers

Dyana kuibuka na Cindy wa Blu 3

0

DYNA

Muziki wa Bongo Fleva Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’.

Na Boniphace Ngumije

UKIAMBIWA utaje tano bora ya wasanii wa kike wanaobamba kunako Muziki wa Bongo Fleva ni wazi utamtaja Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’.

Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo, Dayna ameweza kuendelea kuliweka jina lake masikioni mwa mashabiki wa muziki huu kuanzia Wimbo wa Mafungu ya Nyanya, Nivute Kwako hadi sasa ambapo anabamba na Ngoma ya Angejua aliyoifanyia Studio ya Free Nation chini ya Prodyuza T. Touch.

Katika makala haya ‘Exclusive’, Dayna amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake ya muziki kwa ujumla;

Showbiz; Hongera kwa kazi zako, umeweka nguvu kiasi gani kupushi Wimbo wa Angejua kuhakikisha na wewe unatoboa kimataifa?

Dayna Nyange; Nguvu nimeweka ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuisambaza kwenye media mbalimbali Afrika. Nimeupeleka sehemu nyingi na unafanya poa kama vile Kenya, Kongo, Burundi na pia nimepeleka Trace Music na MTV Base.

Showbiz; Tofauti na muziki una mpango wa kufanya kolabo yoyote na msanii wa nje?

Dayna Nyange; Yaah! Mipango ipo na kwa sasa niko katika mazungumzo na mshkaji wangu Cinderella Santu ‘Cindy’ kutoka Uganda aliyekuwa akiunda Kundi la Blu 3, mambo yakienda poa nitawajulisha wapenzi wa kazi zangu.

Showbiz; Ni kweli Diamond alikuibia mdundo wa Wimbo wa Number One?

Dayna Nyange; Sitapenda kuzungumzia kwa sasa ishu hiyo maana mambo yote tulikwishayaweka sawa.

Showbiz; Kuna madai kuwa unaringa sana hasa linapokuja suala la wasanii kufanya kazi na wewe?

Dayna Nyange; Hapana, watu wananisingizia, unajua kazi na ustaa ni vitu viwili tofauti. Mtu anaweza kutaka kufanya kazi na wewe ili akutumie tu kisa staa na usipate mafanikio yoyote kupitia kazi hiyo. Ukikataa ndiyo maneno hayo kuwa unaringa yanapoanzia.

Showbiz; Kazi zako unaziendeshaje, unamenejimenti?

Dayna Nyange; Hapana sina menejimenti, nakomaa mwenyewe kwa kupigana huku na huko kupitia shoo, kuuza ngoma mitandaoni na vyanzo vingine vya mapato kwa msanii.

Showbiz; Kuna ishu yoyote unafanya tofauti na muziki?

Dayna Nyange; Yap, ninafanya ishu zangu za kijasiriamali za hapa na pale, si unajua tena nina mtoto ambaye sasa hivi anasoma, so inabidi kupambana sana ili kumtimizia mahitaji yake.

Showbiz; Vipi kuhusu uhusiano wako wa mapenzi, unatoka na nani?

Dayna Nyange; Niko single, sina mtu kwa sasa.

Showbiz; Kuna tetesi kuwa hujatulia ndiyo maana hudumu na wanaume?

Dyna Nyange; Si kweli, hayo ni maneno tu ya watu lakini mimi nimetulia na kuwa single ni kwa sababu sijapata tu mtu sahihi!

Showbiz; Unaishi moro au Dar?

Dyna Nyange; Niko Dar kwa sasa maana nilipokuwa moro changamoto ilikuwa kubwa hususan kwenye suala zima la urahisi wa kufanya kazi.

Leave A Reply