The House of Favourite Newspapers

Pah One wamuiga AKA

0

7273faa692L

Boniphace Ngumije

KUNDI la Muziki wa Bongo Fleva, Pah One limefungukia ujio wao mpya wa I Run Dsm kuwa ni idea ambayo wameiiga kutoka kwa staa wa muziki kutoka Afrika Kusini, Kiernan Jarryd Forbes ‘AKA’.

Akizungumza na Showbiz, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Igwe alisema kuwa wanachokifanya ni kama ‘mixtape’ jambo linaloruhusiwa kwa wanamuziki duniani kote.

“Ujue yeye (AKA) ngoma yake inaitwa I Run Jozi akimaanisha I Run Johannesburg lakini kwetu I Run Dar es Salaam lakini hata yaliyomo ni vitu vinavyotofautiana lugha tu ila idea ni moja na wala kwanza hakuna tatizo,” alisema Igwe.

Awali Kundi la Pah One lilikuwa likiundwa na Aika, Nahreel, Igwe na Ola na baada ya hapo likasambaratika ambapo Aika na Nahreel kwa sasa wanaunda Kundi la Navy Kenzo.

Leave A Reply