The House of Favourite Newspapers

Ebitoke Atangaza Rasmi Kung’atuka Kwenye Kundi Lake

MUIGIZAJI wa comedy nchini, aliyejizolea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ (20) ametangaza kujiondoa kwenye kundi lake la Timamu Africa alilokuwa akifanya nalo kazi zake za sanaa.

 

Ebitoke amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameeleza kwamba hatua hiyo imekuja kufuatia mkataba wake na Timamu kumalizika, hivyo ameamua kuondoka ili akafanye kazi sehemu nyingine.

 

“Napenda kuchukua nafasi hii na kuwatarifu Mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, kuanzia sasa nitakua nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV, nikimaanisha mkataba wangu umeisha,” ameeleza Ebitoke.

 

Mbali na kufanya kazi ya uchekeshaji, mwaka huu Ebitoke amecheza filamu yake ya kwanza tangu aanze kuigiza inayoitwa Sema ambayo uzinduzi wake wa awali ulifanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.

 

Aidha, ndani ya TIMAMU, Ebitoke alikuwa akishirikiana na wachekeshaji wengine kama Bwana Mjeshi Mr. Beneficial na Mama Ashura ambaye kitambo hajaonekana na Mkali Wao ambaye alishahama kitambo.


ALICHOKIANDIKA EBITOKE

“Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Management yangu kwa ujumla @timothconrad @timamutv pamoja na wafanyakzi wenzangu @bwanamjeshi @mr_beneficial na @chidi_luba kwa kunilea vema na kufanya nao kazi vizuri na kunifunza mwenendo mzima ambao unapokua msanii unatakiwa uwe nao.

 

“Wamekua wema na wenye UPENDO KWANGU SIKU ZOTE. Pia Napenda kuwashukuru Mashabiki zangu kwa kipindi chote ambapo mmekua mkinisapot na kufurahishamwa na kazi zangu 🙏

 

“Napenda kuchukua nafasi hii na kuwatarifu Mmashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu. Kuanzia sasa nitakua nikifanya kazizangu nje ya Timamu TV Nikimanisha Mkataba wangu na Timamu TV umeisha.

 

“Shukukran ZANGU ZA Dhati kwa Manager wangu 💕 @timothconrad kwa kunilea vyema nitakupenda siku zote Maana bila wewe nisingekua mimi. @bwanamjeshi, @mr_beneficial, @chidi_luba nawashukuru sana kwa upendo mlionao kwangu tangu tumeanza kufanya kazi mpaka sasa, nyie ni familia yangu, tutaendelea kusapotiana kama familia ❤”

EBITOKE: “Haijawahi Kufanyika Bongo, Filamu Kama ya Kwetu”

Comments are closed.