Ebitoke: Hata Kama Nimebabuka, Kileleni Nimechungulia

BAADA ya kuweka picha akiwa amebabuka uso huku maneno ya kejeli yakiwa mengi, msanii wa vichekesho; Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ amesema hata kama amebabuka lakini kileleni mwa Mlima Kilimanjaro amekaribia kufika ‘amechungulia’.

 

Akibonga na Za Motomoto ya Risasi, Ebitoke alisema kuwa alipambana vilivyo ili aweze kufika kileleni mwa mlima huo kwa kuwa alibakisha sehemu ndogo sana, lakini Mungu ni Mwema alipofika anastahili pongezi japo alikuwa kwenye hali mbaya kiafya.

“Ukiiangalia sura yangu haitamaniki hata kidogo lakini ukweli ni kwamba nimefurahi sana, hivyohivyo najua sura yangu itarudi kama kawaida baada ya muda mchache ila ukikutana na mimi sasa hivi natisha jamani,” alisema Ebitoke.

IMELDA MTEMA, DAR


Loading...

Toa comment