The House of Favourite Newspapers

DAWA ZA KULEVYA ZILIVYOTEKETEZWA LAIVU!

Kaimu Kamishna Jenerali, James Wilbert Kaji,  akizungumza na wahabari kabla ya zoezi hilo kuanza.

MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini (DCEA) jana Oktoba 8, 2019,  kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Mahakama, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa , Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), imefanya uteketezaji wa dawa za kulevya ambazo kesi zake zimeshahukumiwa. Akizungumza na waandishi wa habari,  Naibu Kamishna Jenerali James William Kaji,  amesema dawa hizo ni heroini na kokeni ambazo jumla yake ni kilo 120.91. Uteketezaji huo umefanyika katika kiwanda cha saruji cha Wazo Hill jijini Dar.

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga akiingia eneo la tukio kushuhudia.

Akitoa rai katika uteketezaji huo, Kaji amesema kwa serikali ya sasa inayoongozwa na  John Magufuli wale wote waliokuwa wakijihusisha na biashara hiyo haramu waiache mara moja kwani hakuna atakayebaki salama kama ataendelea kuifanya.

Wanahabari waliokusanyika wakati wa uteketezwaji huo walikuwa ni miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo la kihistoria.

Matukio katika picha:

Hapa ni uhakiki wa kila kesi iliyotolewa hukumu na kidhibiti chake.

Mizigo ikiwa tayari kwa kuchomwa
Askari wa ulinzi wakiwa eneo hilo.
Mzigo ukitumbukizwa kwenye moto.

 

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL   

 

Comments are closed.