The House of Favourite Newspapers

Edward Lowassa Aripoti kwa DCI Kuhojiwa

0

Edward Lowassa akiingia ofisini kwa DCI.

 

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili leo, Julai 20 saa mbili asubuhi makao makuu ya Jeshi la Polisi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli zinazodaiwa kuwa ni za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa  Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

 

Edward Lowassa akielekea ofisini kwa DCI.

 

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani  akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.

Polisi wakiimarisha ulinzi eneo hilo.

 

Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

====

LIVE: Ziara ya Kikazi ya Rais Pierre Nkurunzinza Nchini Tanzania

Leave A Reply