The House of Favourite Newspapers

Edwin Van Der Sar Mbioni Kutangazwa Mkurugenzi Man United

Edwin Van Der Sar.

Klabu ya Man United iko katika mpango wa kumtangaza Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo baada ya klabu hiyo kushindwa kufanya vyema katika dirisha kubwa la usajili

Katika mchakato huyo naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward atashirikiana kocha Jose Mourinho kumpata Mkurugenzi huyo wa michezo

Mkurugenzi wa michezo wa As Roma Ramón Rodríguez Verdejo maarufu kama Monchi pia anapigiwa upatu wa kupewa kazi na Man United

Tayari majina matatu yanatajwa kuweza kupewa nafasi hiyo ambao ni Golikipa wa zamani wa timu hiyo muholanzi Edwin Van Der Sar

Pia yupo mkurugenzi wa michezo wa As Roma Muhispania Ramón Rodríguez Verdejo maarufu kama Monchi pamoja na Fabio Paratici.

Comments are closed.