Efm Redio imezindua rasmi msimu wa tatu wa mchezo wa sakasaka. Mchezo huu huchezeshwa kila mwaka na mwaka huu utachezeshwa katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo, Ilala na Bagamoyo. Siku ya leo tarehe 28/05/2017 umezinduliwa rasmi katika kiwanja cha Sinza Tippi wilaya ya Ubungo.
Mchezo huu wa sakasaka huchezeshwa kwa kuficha vitu vyenye thamani ya pesa katika uwanja husika ambapo inampasa msikilizaji afatilie dondoo za kitu hicho pamoja na mahali ili ajue sehemu na aina ya kitu kilichofichwa na atakae kipata atakua mshindi wa pesa taslimu.
Mwaka huu washindi nane katika kila wilaya watajishindia pesa taslimu, ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha shillingi milioni moja akifuatiwa na washindi wa shilingi laki moja na elfu hamsini.