The House of Favourite Newspapers

EFm Yazindua ‘Shika Ndinga’ Kwa Kishindo Kigamboni

Baadhi ya washiriki wa shindano la Shika Ndinga wakishiriki shindano hilo kwa kuishika gari husika.
Meneja Mkuu wa Efm Redio, Dennis Ssebo, akizungumza jambo kabla ya mashindano kuanza.
Washindi wa Shika Ndinga katika Wilaya ya kigamboni, Joyce Daniel na Salum Yusuph wakiwa kwenye pikipiki zao.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.
Washindi wa pikipiki wakipozi baada ya kumalizika kwa mchezo.

Na HilalyDaudi/GPL

KITUO cha Redio cha Efm kwa mara nyingine tena kimekuja na shindano la ‘Shika Ndinga’ ambalo litawashindanisha wakazi wa wilaya sita za Mkoa wa Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umefanyika jana katika viwanja vya Machava Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Tunatoa pikipiki 12 katika wilaya sita, kila wilaya tunatoa pikipiki mbili kwa Kigamboni, Temeke, Ilala, Kinondoni, Bagamoyo na Kibaha ambapo mwisho wa mashindano tutatoa magari mawili aina ya Suzuki Cary,” alisema Meneja Mkuu wa Efm, Dennis Ssebo.

Pikipiki mbili zinazotolewa kwa kila wilaya kila moja itachukuliwa na mwanamke atakayeweza kushikilia ndinga (gari) hadi mwisho kwa kuzingatia vigezo vilivyopo. Na pikipiki nyingine itakwenda kwa mwanamme atakayeshinda mtihani wa kushikilia ndinga kulingana na masharti yaliyopo.

Lengo kubwa ni kusaidia jamii kwani soko letu ndiyo mtaji wao kwa kusikiliza Redio Efm ambapo wanapata mtaji kupitia zawadi tunazotoa kwani ni zawadi ambazo watatumia kama biashara za kuwaingizia kipato,” alisema Ssebo.

Katika ufunguzi wa mashindano hayo, washindi walioibuka kidedea kwa kujinyakulia pikipiki mbili ndani ya wilaya ya Kigamboni baada ya kushika ndinga hadi mwisho wakiwabwaga wengine, ni Joyce Daniel na Salum Yusuph.

 

Comments are closed.