The House of Favourite Newspapers

EL CLASICO: BARCELONA YAITWANGA MADRID 5-1

KLABU ya Barcelona imeishushushia kipigo cha aina yake mahasimu wao, Real Madrid baada ya kuwafunga mabao 5-1 katika mechi ya La Liga maarufu kama El Clasico jana jioni.
Barcelona iliyokuwa nyumbani Camp Nou, imeshinda kwa mabao hayo matano huku mshambuliaji wake kutoka Uruguay, Luis Suarez akipiga hat trick.

Mechi hiyo ilionekana mapema kuwa ya Barcelona baada ya Coutinho kuanza kufunga kabla ya Suarez kuongeza bao la pili.
Lopetegui huenda ukawa mwisho wake, Real Madrid.
Lakini Madrid walianza kipindi cha pili kwa kasi kupata bao la mapema kupitia Marcelo lakini ikawa kama wameichokoza Barcelona ambayo ilianza kufunga mfululizo, Suarez akifunga mabao mengine mawili na mkongwe, Artulo Vidal akifunga dakika chache baada ya kuingia uwanjani.

Marcelo amefunga kwa mara 3 mfululizo kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kuichezea Madrid.

Sergio Ramos jana ametimiza vipigo 20 kutoka kwa FC Barcelona- amefungwa mara 18 katika Clasico na mara mbili akiwa na Sevilla. Hakuna mchezaji aliyepoteza mechi nyingi za El Clasico kumzidi El Capitano Sergio Ramos.

El Clasico hiyo ilikuwa maarufu zaidi kwa maana ya kuwakosa nyota wawili, Cristiano Ronaldo aliyehamia Juventus na Lionel Messi ambaye ni majeruhi.

Salamu za Rais Magufuli, RC Makonda msibani kwa Isack Gamba

Comments are closed.