The House of Favourite Newspapers

El da Bway Akana Kuwa na Bifu na Nahreel

0
El da Bway.

KWA mara ya kwanza prodyuza kutoka Home Town Records, El da Bway amefungukia bifu lake na aliyekuwa prodyuza wa studio hiyo, Nahreel kuwa wapo sawa na hawakuwa na bifu kama watu walivyokuwa wakishadadia.

 

El da Bway.

 

Akipiga stori mbili-tatu na Showbiz, El da Bway ambaye kwa muda mrefu amekuwa akimtengenezea ngoma staa wa R&B, Rama Dee alisema, tangu ameachiwa kuiongoza studio hiyo mwaka 2015, wengi walikuwa wakimsema kuwa aliibua bifu na Nahreel jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.

 

Nahreel.

 

“Tangu nimeingia Home Town nimekutana na vingi sana. Kuondoka kwa Nahreel hakujatokana na mimi. Naongea naye vizuri na hatujawahi kuwa na bifu. Kwa sasa naimba na yeye anaimba hivyo yaani,” alisema El da Bway licha ya kuwa prodyuza, anatikisa na Ngoma ya Boss.

 

SHOWBIZ | IJUMAA WIKIENDA

Leave A Reply