The House of Favourite Newspapers

ELEWA TATIZO LA MIKONO / MIGUU KUFA GANZI

KATIKA mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kufa ganzi kwa viungo vya mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu huitwa Peripheral Neuropathy.  

 

Matatizo haya ya kiafya ya miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika.

 

DALILI

Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo: Mtu kuhisi ganzi, kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika, maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni au mikononi. Miongoni mwa mambo ambayo husababisha neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

 

Kupungua kwa virutubisho mwilini, hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex), matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na Virusi vya Ukimwi, uzito mkubwa wa mwili, ugonjwa wa kisukari, (diabetic polyneuropathy) na shinikizo la damu. Kufa ganzi katika mikono na miguu kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu kadhaa, hasa za mishipa ya neva kuwa na matatizo.

 

Mikono au miguu kuhisi kama inachomwa sindano (Paresthesia) ni moja ya dalili ya ganzi. Ganzi ya mikono na miguu husababishwa na kuwa na lishe duni kwa ugonjwa au mishipa ya neva kuwa na hitilafu na machafuko ya mfumo.

 

Upungufu wa vitamini muhimu kama B5 vitamini, B6 na B12, vitamini A na vitamini D unaweza kusababisha kupata ganzi ya mikono na miguu. Kwa hiyo ni muhimu sana kula vitamini kwa ajili ya kutibu ganzi ya miguu na mikononi.

 

Ganzi katika mikono na miguu ni dalili muhimu ya ugonjwa wa kisukari, hasa aina ya II kisukari ambayo husababisha mfumo wa neva malfunction na hatimaye husababisha uharibifu wake. Ganzi katika mikono na miguu wakati umelala ni dalili muhimu ya multiple sclerosis, hasa wakati wa hatua yake ya awali. Multiple Sclerosis inasababisha uharibifu wa neva, pia kitaalamu inajulikana kama neurodegeneration.

Syndrome Raynaud ni machafuko katika damu kutokana na joto kuwa chini sana kunakosababishwa na spasms ambazo huzuia au kukataza mtiririko wa damu wa kawaida mwilini hasa kuelekea kwenye vidole na miguuni hali ambayo inaongeza ganzi katika vidole vya mikononi na miguuni. Kuna kitu kinaitwa kitaalamu Carpal syndrome, hii husababishwa na kuumia kwa neva kuzunguka mkono na huweza kuleta ganzi sehemu hiyo.

 

Mishipa ya ateri ikiwa na hitilafu pia husababisha ganzi ya mikono na miguu. Kifupi ni kwamba kuna sababu nyingi za ambazo zinaweza kusababisha hisia ya ganzi katika mikono na miguu. Baadhi ya hizo ni pamoja, kuumwa na wadudu au wanyama, athari za aina fulani ya dawa, kunywa pombe kupita kiasi, uvutaji wa tumbaku au sigara na kadhalika.

 

TIBA NA USHAURI

Kuondoa ganzi katika mikono na miguu itahitaji matibabu ambayo yatatolewa na mtaalamu baada ya kujua chanzo cha hali hiyo kutokea kwani kama tulivyoona hapo juu, sababu za maradhi haya zipo nyingi.

 

Lakini hali hiyo ikianza kujitokeza unawea kufanya masaji eneo husika kwa kuikandakanda kama huduma ya kwanza. Kufanya hivyo huboresha mzunguko wa damu, na kusababisha ongezeko katika mtiririko wa damu kwenye mishipa na hivyo inaweza kuondoa ganzi. Uonapo dalili hizo nenda kaonane na wataalamu wa afya kwa ushauri hasa kuhusu lishe na matibabu.

Comments are closed.