The House of Favourite Newspapers

Elias Maguri alia na kusimama Ligi Kuu Bara

0

maguri stars sauzMshambuliaji wa Stand United, Elias Maguri.

Khadija Mngwai,Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa Stand United, Elias Maguri, amefunguka kwa kusema kuwa mapumziko ya mara kwa amra katika ligi yanachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha kasi ya wachezaji.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar ambapo kabla ya hapo, ilisimama kwa muda wa mwezi mmoja kupisha timu ya taifa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Maguri amefunguka kuwa kwa sasa anajipa tizi la peke yake kwa ajili ya kuimarisha kiwango chake na kudai kuwa mapumziko ya mara kwa mara yanaathiri viwango vyao.

“Mapumziko ya mara kwa mara yanachangia kushusha viwango vyetu kwa kuwa kila mara tunakuwa tunaanza upya, nafikiri hivi siyo vizuri.

“Kwa upande wangu nimekuwa nikijipa mazoezi binafsi hadi hapo nitakapoungana na timu yangu baada ya mapumziko mafupi ya kuanza maandalizi ya ligi.“Lengo ni kuhakikisha nafanikiwa kuwa katika kiwango kizuri kuisaidia timu yangu kuweza kumaliza katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi,” alisema Maguri.

 

 

 

Leave A Reply