The House of Favourite Newspapers

Kerr : Mabeki wangu hawana uzoefu

0

Dylan-KerrKocha  Wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr.

Omary Mdose,Dar es Salaam
KOCHA Wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amewakingia kifua mabeki wake wa kati, Mohammed Fakhi na Novatus Lufunga kwa kusema makosa wanayoyafanya kwa sasa yanatokana na kukosa uzoefu.

Simba ambayo ipo visiwani Zanzibar ikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, juzi Jumatatu ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Jamhuri, huku mabeki hao wakionekana kufanya makosa yaliyowapa mabao wapinzani wao.

Lufunga alijiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo akitokea African Sports huku Fakhi akisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea JKT Ruvu, wote kwa pamoja huo ulikuwa mchezo wao wa kwanza wa kimashindano.

“Makosa ya mabeki wangu wa kati ndiyo yametugharimu, lakini hawapaswi kulaumiwa sana kutokana na kwamba hawana uzoefu, hivyo wanahitaji muda zaidi wa kuwa fiti.

“Kama nilivyosema awali kabla ya kuja huku Zanzibar kwamba michuano hii ninaitumia kwa ajili ya kutoa nafasi kwa kila mchezaji wangu, hivyo nimepanga kuwapa tena nafasi ili nione tena uwezo wao,” alisema Kerr.

Leave A Reply