The House of Favourite Newspapers

Elimu Na Tamisemi Kuja Na Mikakati Wanafunzi Shule Zilizokumbwa Na Mafuriko Kuendelea Na Masomo

0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda akiongea jambo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda amesema Serikali itahakikisha inaweka mazingira ya wanafunzi wote ambao shule zao zimeathirika na mafuriko nchini kuendelea na masomo.

Amesema hayo Aprili 15, jijini Dodoma katika kikao kati ya Uongozi wa Wizara hiyo na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kilichokuwa na lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa Mageuzi ya Elimu kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo na Mitaala iliyoboreshwa na kuongozwa na Mawaziri wa Wizara hizo.

” tumekutana kwa ajili ya utekelezaji Sera lakini kubwa lililo mbele yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunawezesha wanafunzi waliokwama kuendelea na masomo kutokana na athari za mafuriko nchini wanawezeshwa kuendelea na hii ni kwa shule zote na setikali na binafsi.” Amesema Mkenda

Mawaziri hao wameagiza wataalamu kupata taarifa za tathmini kutoka kwa Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu walio katika maeneo mbalimbali nchini na maeneo mengine waweze kufika na kuja na mipango ya muda mfupi na mrefu ya kutekeleza agizo hilo ikiwemo upatikanaji rasilimali.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Mchengerwa amesema wataalamu wanapaswa kuandaa maandiko ya upatikanaji fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo ambao wako tayari.

Leave A Reply