The House of Favourite Newspapers

ELIMU YATOLEWA KUPAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI

Bi. Elizabeth Mratibu wa taasisi ya Newhope Tanzania

Wakati Taifa linajiandaa kwenda katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, elimu imetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kwa kupiga kura za kuchagua Viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali haki za Watoto wa Kike. Hayo yameelezwa jana na Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za mtoto wa kike la New Hope Tanzania, Bi. Elizabeth Ngaiza ambapo alisema Katika Kampeni ya “Niache Nisome Kwanza” anayoendesha amebaini uwepo wa baadhi ya viongozi wa Ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi kusimama katika nafasi yao kutetea haki za mtoto wa kike.

“Lengo la Kampeni ya Niache Nisome Kwanza ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo vyovyote,” alisema Bi. Elizabet.

Hata hivyo Bi. Elizabeth amewaomba wadau na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika Kampeni ya Kumlinda mtoto wa kike apate elimu Bora kwa kuwa anaamini ukimwezesha mwanamke kupata elimu itasaidia kuinua kipato cha Familia na Taifa kwa ujumla.

Imeandaliwa na Neema Adrian/GPL

Comments are closed.