The House of Favourite Newspapers

Elon Musk Akana Tuhuma za Kutoka Kimapenzi na Mke wa Mwanzilishi wa Google

0

 

Bilionea namba moja duniani, Elon Musk amekana tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na  Nicole Shanahan, ambaye ni mke wa mwanzilishi wa Google, Sergey Brin.

 

Kauli ya mmiliki huyo wa kampuni ya magari ya uneme ya Tesla, imekuja baada ya ripoti katika Jarida la Wall Street kieleza kwamba urafiki wa Musk na Brin ulikufa kutokana na madai ya Musk kuwa na uhusiano na mke wa Brin.

 

Kupitia mtandao wa Twitter, Musk alitoa maoni yake katika jarida la Wall Street, akisema ripoti hiyo ilikuwa “Upuuzi mtupu”, kwamba urafiki wake na Brin haujafa, na kwamba “Walikuwa kwenye hafla pamoja jana usiku.”

 

Gazeti la Wall Street Journal lilibaini kuwa liliegemea ripoti yake kwenye vyanzo vya habari, likisema kwamba mwaka jana Musk alikuwa akichumbiana na Shanahan.

 

Hii ilisababisha Brin kuanzisha kesi ya talaka mapema mwaka huu na kufuta urafiki wa muda mrefu kati ya wakuu hao wawili wa teknolojia, jarida la Wall Street lilisema.

 

Lakini Musk aliandika ujumbe kwenye Twitter, “Kwa miaka mitatu, nimemuona Nicole mara mbili tu, na katika matukio hayo mawili kumekuwa na watu wengi karibu. Hakuna kitu cha kimapenzi.”

Leave A Reply