Basi la Shule Lapata Ajali na Kusababisha Vifo vya Watu 10, Rais Atuma Salamu za Pole

Basi la Shule ya King David likiwa limetumbukia mtaroni katika eneo la Mikindani, Mtwara

 

BREAKING: Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kufuatia basi la wanafunzi wa Shule ya King David Mtwara lenye namba za usajili T 207 CTS lililopata ajali asubuhi ya leo Jumanne, Julai 26, 2022 eneo la Mikindani Mtwara likiwa na wanafunzi na kuua watu 10 wakiwemo wanafunzi nane wa shule hiyo.

 

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Samia ameandika: “Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa Shule ya Msingi ya King David na watu wazima 2 vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kutumbukia shimoni. Nawapa pole wafiwa, mkuu wa mkoa na jamaa. Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu na kuwaponya majeruhi.

 

Taarifa za awali zinaeleza kuwa takribani watu 19 wamejeruhiwa katika ajali hiyo na wamekimbizwa katika Hospitali ya Ligula wanakoendelea na matibabu.

 

Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitakujia hivi punde.

 

Mashuhuda wakilitazama basi la Shule ya King David likiwa limetumbukia mtaroni katika eneo la Mikindani, Mtwara

 

Basi la Shule ya King David likiwa limetumbukia mtaroni katika eneo la Mikindani, Mtwara

 

Basi la Shule ya King David likiwa limetumbukia mtaroni katika eneo la Mikindani, Mtwara

 3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment