The House of Favourite Newspapers

ENGLAND YATINGA ROBO FAINALI KIBISHI

ENGLAND wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kushinda kwa penalti 4-3 MOSCOW, Urusi baada ya sare ya bao 1-1 kwa dakika 120. Harry Kane alikuwa wa kwanza kuifungia England bao katika kipindi cha pili mwanzoni, lakini Colombia wakasawazisha kwenye dakika tano za nyongeza.

 

Awali England ilikuwa haipewi nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye fainali za mwaka huu, lakini mwendo wao wa sasa umekuwa wa kasi ya hali ya juu na kuwa tishio. Sasa ina maana kuwa England bado hawana uhakika wa kwenda hatua ya nusu fainali kwa kuwa wanakutaka na Sweden kwenye mchezo wa robo fainali, timu ambayo iliitoa Uswisi kwa kuichapa bao 1-0, jana jioni.

Katika mchezo wa England, ambao ulijaa ubabe wa hali ya juu huku zaidi ya wachezaji wa Colombia watano wakipewa kadi za njano, Kane alifanikiwa kuifungia timu hiyo bao katika dakika ya 57 kwa mkwaju wa penalti. Hili ni bao la sita kwa staa huyo wa Tottenham Hortspur, kwenye fainali za mwaka huu akiwa ameweka rekodi ya mchezaji raia wa England aliyefunga mabao mengi kwenye fainali moja, lakini kwa sasa akiwa ndiye kinara wa ufungaji.

 

Hata hivyo, wakati England wakijiandaa kushangilia kutinga kwenye hatua ya robo, dakika tano za nyongeza zilitosha kwa Yerry Mina, kuisawazisha Colombia kwa kichwa na kuifanya mechi hiyo kwenda kwenye dakika 30 za nyongeza.

Katika dakika hizo 30, Colombia waliendelea kutawala mchezo huo huku wakati wa mapumziko wakipewa mawazo na mshambuliaji wao staa, James Rodriguez ambaye anasumbuliwa na majeraha lakini hayakutosha kuwaondoa na ushindi.

Kwenye mikwaju ya penalti England walifunga kupitia kwa Kane, Marcus Rashford, Trippier na Dier huku Henderson akikosa na Colombia walifunga kupitia wa Radamel Falcao, Cuadrado, Muriel na  Uribe na Bacca wakikosa mikwaju yao.  Hii ni mara ya kwanza England wanafuzu kwa hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya penalti kwenye Kombe la Dunia.

Colombia (4-3-2-1): Ospina; Arias (Zapata 115), Davinson Sanchez, Mina, Mojica; Barrios, Carlos Sanchez, Lerma (Bacca 61); Juan Cuadrado, Quintero (Muriel 87); Falcao

Subs not used: Murillo, Aguilar, Vargas, Uribe, Diaz, Izquierdo, Jose Cuadrado 

Goals: Mina 90 

Booked: Barrios, Arias, Carlos Sanchez, Falcao, Bacca. Juan Cuadrado

Manager: Jose Pekerman

England (3-5-2): Pickford; Walker (Rashford 112), Stones, Maguire; Trippier, Henderson, Lingard, Alli (Dier 80), Young (Rose 102); Sterling (Vardy 87), Kane

Goal: Kane 57 (pen)

Booked: Henderson, Lingard

Subs not used: Butland, Welbeck, Cahill, Jones, Loftus-Cheek, Alexander-Arnold, Pope

Manager: Gareth Southgate

Attendance: 44,190

Comments are closed.