The House of Favourite Newspapers

ENGLAND YATOA KICHAPO KIKALI KOMBE LA DUNIA

Timu ya Taifa ya England leo Jumapili imefanikiwa kutinga hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Panama mabao 6-1 katika mchezo uliokuwa wa upande mmoja wa Kundi Ghuko Moscow, Urusi.

 

Kwa matokeo haya, England imefuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Ubelgiji ambao nao wamefuzu hatua inayofuata. Timu zingine zilizopo kwenye Kundi G ni Tunisia na Panama zenyewe zimeshatolewa kutokana na kutoshinda mchezo wowote, hawa watakutana kwenye mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba.

Kapteni wa timu ya taifa ya England, Harry Kane akipiga penalti dhidi ya Panama
Harry Kane (kushoto) na Jordan Henderson wakishangilia moja ya mabao.
Mchezo ukiendelea.
Mashabiki wa England wakifuatilia mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Novgorod nchini Urusi.

Mashabiki wakishangilia wakiwa mitaani wakati wa mechi.

Mashabiki wa England waliokuwa wakifuatilia mchezo huo wakishangilia baada ya timu yao kupata bao.

Comments are closed.