The House of Favourite Newspapers

ads

Erik ten Hag: Manchester United Watanyanyua Taji Msimu Huu

0
Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag.

KOCHA wa Manchester United, Erik ten Hag alisema kwamba timu yake ina nafasi nzuri ya kushinda taji lao la kwanza tangu 2017 msimu huu.

Ten Hag aliyasema hayo wakati wanajiandaa kwa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Nottingham Forest juzi ambao walishinda mabao 3-0.

United imekosolewa na mashabiki wao kwa ukame wa vikombe kwenye klabu hiyo, huku timu hiyo ikiwa na mataji ya Ligi ya Europa na Kombe la Carabao, waliyotwaa mwaka wa 2017.

United wameimarika chini ya Ten Hag na ndio timu pekee ya Uingereza iliyosalia kwenye mashindano manne tofauti msimu huu. Premier League, Carabao Cup, FA Cup na Europa League.

Leave A Reply