The House of Favourite Newspapers

Esma: Wakisema Nimeachwa, Naongeza Ndinga

0

ESMA Khan ambaye ni dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Mondi’ amesema wakati watu wakiwa bize kumsema ameachika, yeye yuko bize kununua ndinga nyingine mpya.

 

Akibonga na OVER ZE WEEKEND, Esma alisema watu wako bize kumsema kwamba ameachwa na aliyekuwa mumewe, Petit Man, lakini yeye anapiga kazi na kupata pesa ambazo zimemwezesha kufanya anachotaka.

 

“Eti kuachika wanaona kama kitu kipya kwenye maisha, lakini mimi niseme hivi, wakiwa wanaendelea kunisema bila kujua undani wa mambo, kazi yangu ni kununua ndiga nyingine mpya maana ni kitu ninachokipenda, sisikilizi yasiyokuwa na maana kwangu kwa sababu hata kama nimeachika maisha yanandelea,” alisema Esma.

 

Esma na Petit walikiri kurudiana hivi karibuni kwani walikuwa wameachana kwa muda mrefu, lakini sasa wameachana tena.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply