The House of Favourite Newspapers

ESTER ATESWA NA UBONGE NYANYA

Ester Kiama

MSANII wa filamu za Kibongo, Ester Kiama amefunguka kuwa hakuna kitu kinachomtesa katika maisha yake kama ubonge alionao kwa sasa.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Ester alisema siku za hivi karibuni amekuwa akinenepeana bila mpangilio bila kujua ni kitu gani kinachosababisha na kujikuta akijichukia mwenyewe kutokana na mwili mkubwa alionao.

“Kiukweli nauchukia sana mwili wangu kutokana na ubonge huu nilionao na sijui unatoka wapi na haya maisha magumu hivi, nimeanza kwenda gym kwa ajili ya kupunguza unene naamini ipo siku nitarudi kwenye mwili wangu ule wa zamani,” alisema Ester.

Comments are closed.