The House of Favourite Newspapers

TIKO SANAA BILA KIKI INAWEZEKANA

Tiko Hassan

STAA wa muziki na filamu Bongo, Tiko Hassan ametoa ya moyoni na kueleza kwamba sanaa bila kiki inawezekana japokuwa wasanii wengi wamejikuta ‘wakilemaa’ na kiki zisizokuwa na maana.

Akichezesha taya na Za Motomoto News, Tiko alisema wasanii wa sanaa mbalimbali wanatakiwa kujifunza kwamba kufanya kiki hakusaidii kitu chochote kwenye sanaa yao bali wanatakiwa kutumia maarifa hayo ya kiki na akili zao zote katika kutengeneza kazi nzuri.

“Kiki siyo ishu kwangu, naamini katika kufanya kazi nzuri maana kwa sasa nimejikita zaidi kwenye kutengeneza kazi bora na kweli nimefanikiwa kwani kazi yangu ya Lambalamba inafanya vizuri sana na sijafanya kiki yoyote,” alisema Tiko.

Comments are closed.