The House of Favourite Newspapers

Etihad Yasherehekea Miaka 10 ya Usafiri wa Anga

0

EY-Etihad-Airways-new-logo-En

  • Safari tano kwa siku ikiwamo za alfajiri kwa wasafiri wote wa Abu Dhabi na Qatar
  • Nyongeza ya safari za jioni kwa kipindi za kiangazi ikiwa ni maalumu kwa wafanyabiashara na wasafiri wanaoenda kutembea

Shirika la Ndege la Etihad limesherehekea miaka 10 ya huduma ya usafiri wa anga kwa kuzindua safari tisa za ndege kutoka Abu Dhabi – Doha kipindi hiki cha kiangazi ikitimiza ahadi yake kuwa shirika bora la usafiri katika ukanda huo wa Gulf kibiashara.

Kuanzia 1 Agosti 2016 shirika hili litaongeza safari za wiki kuelekea mji mkuu wa Qatar. Safari mpya za ndege za alfajiri pamoja na jioni siku ya Alhamisi na Jumamosi zitawawezesha wasafiri ambao ni wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati kati ya Abu Dhabi na Doha.

Safari hizo mpya zitawawezesha wasafiri kutoka Doha kuwa na chaguo la usafiri wa ndege za Shirika la Etihad zinazofanya safari zake maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati, Ulaya, Afrika, Asia, na Amerika Kaskazini.Huduma hiyo mpya inaendana na kipindi hiki cha miezi ya kiangazi ambacho huwa na ongezo idadi ya wasafiri.

Tangu kuanzishwa safari za Doha mwaka 2016, Shirika la Ndege la Etihad limekuwa likiboresha huduma zake ili kuendana na mahitaji halisi ikiwamo kuiunganisha dunia na huduma mbalimbali zinazopatikana Abu Dhabi.

Makamu wa Rais  wa Masoko katika Shirika la Ndege Etihad, Daniel Barranger alisema, “Qatar ni kitovu cha biashara kwa Shirika la Etihad. Tangu 2006 kumekuwapo maendeleo mazuri ya safari za ndege nne kwa siku kati ya Abu Dhabi na Doha, ndiyo sababu tunasherehekea kumiza miaka 10 kwa kuunganisha miji hii mikuu miwili kwa kuongeza safari za ndege tisa kila wiki ikiwa ni kuonyesha dhamira yetu kukuza biashara Doha.”

Aliongeza kuwa, “Kwa kuboresha safari zetu kwenda na kurudi Doha, tumejenga mtandao imara na ni matumaini yetu wateja wetu watakuwa na wigo mpana wa kuchagua usafiri muda unaomfaa kwenda Abu Dhabi.”

Wageni wanaosafiri kwenda Abu Dhabi watakuwa na fursa ya kupanga na kuchagua ndege aipendayo kufika Ulaya, ikiwamo miji ya London, Manchester, Paris, Dublin, Rome, Munich, Milan, Geneva, Madrid, Athens na Istanbul.  Pia, Delhi, Mumbai, Kathmandu, Dhaka, Calicut, Cochin pamoja na Hyderabad miji inayounganisha India.

Pia mteja anaweza kusafiri kwa ndege ya shirika la Etihad kutokea Doha na kutembelea miji mbalimbali ya USA; – New York, Chicago, San Francisco, Los Angeles, Washington  na Dallas.

Wasafiri pia watapata huduma ya kipekee ya US Pre-Clearance immigration and customs wakiwa katika uwanja wa ndende wa kimataifa wa Abu Dhabi.

Hii humwezesha msafiri anapowasili Marekani kama msafiri wqa ndani kumpuguzia muda ambao angetumia kushughulikia na kukamilisha. masuala ya uhamiaji na taratibu za kuwasili.

Safari za kila siku kati ya Abu Dhabi and Doha. Ratiba mpya ya usafiri wa ndege utakaoanza tarehe 1 Agosti, 2016

 Flight no. Origin Destination Departs Arrives Aircraft Frequency
  EY 399 Abu Dhabi Doha 02:50 02:55 A320 Daily
  EY 390 Doha Abu Dhabi 04:00 06:15 A320 Daily
  EY 331 Abu Dhabi Doha 07:45 07:50 A320 Daily
  EY 332 Doha Abu Dhabi 08:50 11:05 A320 Daily
    EY 393 Abu Dhabi Doha 08:45 08:50 A321 Daily
   EY 394 Doha Abu Dhabi 09:55 12:10 A321 Daily
  EY 395 Abu Dhabi Doha 15:30 15:35 A321 Daily
  EY 396 Doha Abu Dhabi 16:45 19:00 A321 Daily
  EY 353 Abu Dhabi Doha 17:30 17:35 A320 Thur & Sat
  EY 354 Doha Abu Dhabi 18:35 20:50 A320 Thur & Sat
   EY 391 Abu Dhabi Doha 21:35 21:40 A320 Daily
  EY 398 Doha Abu Dhabi 22:50 01:05 A320 Daily

NB: SAFARI ZOTE ZA KUWASILI NA KUONDOKA NI KWA MUDA WA ENEO HUSIKA.

Nauli zote zinafanyiwa booking kwa njia ya mtandao wa etihad.com, au ofisi ya Shirika la Ndege Etihad au wakala wa eneo ulilopo aliyeidhinishwa na Etihad.

KUHUSU SHIRIKA LA ETIHAD

Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad  ni linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya shughuli zake; kupitia Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.

Shirika limewekeza kwenye mashirika nane; : Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia, na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya kazi kama  Etihad Regional.

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Makao makuu yake yakiwa Abu Dhabi, Shirika la Etihad limetangaza malengo ya kuhudumia abiria 117 na mizigo Mashariki ya KATI, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Amerika. Shirika lina ndege za Airbus na Boing 122, ikiwa na zingine 204 ambazo bado zinatumika kwa sasa; , ikiwamo  71 Boeing 787s, 25 Boeing 777Xs, 62 Airbus A350s and 10 Airbus A380s

Kwa maelezo zaidi 

Updesh Kapur

MENEJA MAWASILIANO SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD

Direct: +971 2 511 3276

Mob:   +971 5 6546 1402

Email: [email protected]

Leave A Reply