The House of Favourite Newspapers

EU Yataka Suluhu ya Amani Nchini Kenya Baada ya Matokeo ya Uchaguzi

0
Raila Odinga na William Ruto

BAADA ya matokeo ya uchaguzi, Raila Odinga amejitokeza na kukataa matokeo hayo kwa kusema yalikuwa na kasoro hivyo kutotambua uteuzi wa William Ruto na kuahidi kukata rufaa ya kupinga matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya Kenya.

 

Muungano wa nchi za Ulaya (EU) umewataka wakenya kutafuta suluhu ya amani ambayo haitaleta madhara kwa jamii ya watu wa Kenya.

Mwakilishi Mkuu wa EU Josep Borrell

EU imewataka Wakenya kutatua matatizo yaliyobaki kwa kutumia sheria.

 

Mwakilishi Mkuu wa EU Josep Borrell alisema:

 

Taarifa hiyo ilikuwa ikisema “imezingatia matokeo ya Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), kumtangaza Bw William Ruto kuwa mshindi wa uchaguzi na uamuzi wa kukata rufaa wa Bw Raila Odinga”

Umoja wa Ulaya umempongeza Rais Mteule wa Kenya William Ruto

Viongozi wote wa kisiasa na kijamii lazima waepuke vurugu zozote na watoe wito wa utulivu. Ni wakati wa uongozi wa kisiasa na wajibu kutoka kwa wale wote wanaohusishwa na mchakato wa uchaguzi,”

 

Pamoja na hayo lakini bwana Josep Borrell amempongeza Raisi mteule William Ruto.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick Kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply