The House of Favourite Newspapers

Euro 2016: Ujerumani Yatinga Nusu Fainali

0

Ujerumani VS Italia (3)

Ujerumani wakishangilia kutinga nusu fainali.

Ujerumani VS Italia (1)

Wachezaji wa Italia wakiwa hoi baada ya kipigo kutoka kwa Ujerumani.

Ujerumani VS Italia (4)

Matteo Darmian wa Italia akipiga penalti ya mwisho iliyookolewa na Manuel Neuer.

Ujerumani VS Italia (2)

Kipa wa Ujerumani, Manuel Neuer akiokoa penalti ya Matteo Darmian wa Italia.

 

Ujerumani VS Italia (5)

Leonardo Bonucci akiifungia Italia penalti.

Ujerumani VS Italia (7)

Simone Zaza akipiga penalti iliyotoka nje.

Ujerumani VS Italia (6)

Zaza baada ya kukosa penalti.

TIMU ya Taifa ya Ujerumani usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya EURO 2016 baada ya kuichapa timu ya Italia kwa penalti 6-5 baada ya matokeo ya 1-1 katika dakika 120.

Katika mechi hiyo ya robo fainali iliyopigwa huko Bordeaux nchini Ufaransa timu ya Ujerumani ndiyo iliyotangulia kupata bao kupitia kwa Mesut Ozil dakika ya 65 kabla ya Italia kusawazisha katika dakika ya 78 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Leonardo Bonucci baada ya beki wa Ujerumani Jerome Boateng kunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Waliopiga penalti ni hawa;

matuta

Baada ya muda wa nyongeza kumalizika ziliamriwa kupigwa penalti ambapo Ujerumani waliibuka kidedea kwa penalti 6-5.

Leave A Reply