The House of Favourite Newspapers

Ewura Yataja Chanzo cha Mlipuko wa Gesi Moro

0

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, Titus Gaguo amebainisha chanzo cha mlipuko wa gesi uliotokea jana Msamvu na kusababisha majeraha kwa watu watano wakiwemo wanahabari wa StarTV, Abood, Imani FM na Global Publisher wa mkoani humo ambao walifika katika eneo hilo baada ya kupata taarifa ya kutoka kwa mlipuko uliosababishwa na mitungi ya gesi kwenye nyumba hiyo.

“Tulitoka haraka na vifaa vyetu kuwahi eneo la tukio, tulipofika tukakuta nyumba inateketea kwa moto, kwa mujibu wa mashuhuda walisema chanzo ni kulipuka kwa mitungi ya gesi iliyokuwa imetunzwa humo, wakati tunaendelea kuripoti ulilipuka mtungi mwingine uliyokuwa karibu yetu.” alisema mmoja wa waandishi wa habari aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Leave A Reply