The House of Favourite Newspapers

#Exclusive: Dinamite Binti Anayeishi Itali – ”Diamond Nampenda, Kupika Sijui Ila Kula Najua” – Video

0

Binti mdogo wa Kitanzania anayeishi nchini Italia, anayekuja kwa kasi kwenye gemu la muziki wa kizazi kipya, Namite Liesbeth Selvaggi @dinamite_tz amesema bado ndoto za kukutana na staa wa Bongo Fleva, @diamondplatnumz ziko palepale huku akieleza kwamba anampenda sana msanii huyo na anaamini ipo siku watafanya kazi pamoja.

“Bado sijakata tamaa na sitakata tamaa mpaka nitakapoonana na kuzungumza naye, nampenda sana,” alisema Di Namite kwenye mahojiano na Exclusive za Imelda Mtema.

Tayari binti huyo mdogo anayesimamiwa kimuziki na mama yake @mbambavanessa ameshaachia kazi kadhaa, ikiwemo Rafiki alioshirikiana na Barnaba Classic, Tamaduni pamoja na ngoma yake mpya ya Mjomba inayofanya poa Youtube.

Leave A Reply