The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: KOCHA GOR MAHIA AMFUATA BANDA SAUZI

ALIYEKUA kuwa Kocha wa Gor Mahia FC ya Kenya, Dylan Kerr (51), ametangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Black Leopards inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini kuchukua mikoba ya  Joel Masutha ambaye alikuwa akiinoa timu hiyo.

 

Kerr ambaye aliwahi kuifundisha Simba Sc ya jijini Dar es salaam msimu wa 2015–2016, kabla ya kutimkia Gor Mahia, amemalizana na klabu hiyo ambayo inashiriki ligi ya nchini humo ambayo Beki wa Taifa Stars, Abdi Banda anacheza pia kwenye timu ya Baroka FC inayoshiriki ligi hiyo.

 

Kocha huyo Raia wa Uingereza alieleza kuachana na Gor Mahia kutokana na kupata dili hilo baada ya kuelewana na mabosi wake kisha kuelekea zake Afrika Kusini.

 

Muingereza huyo atatambulishwa rasmi siku yoyote kuanzia leo ndani ya klabu hiyo iliyo nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa imecheza mechi 11.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Banda ambaye pia amewahi kuichezea Simba enzi za kocha huyo klabuni hapo, ame-post picha akiwa na Kerr na kuandika, “Baada ya miaka mitatu hatimaye tumekutana tena.”

TBC1: Baada ya Kipigo Lesotho, Taifa Stars Warejea Nchini

Comments are closed.