EXCLUSIVE: NAPE Afungukia ‘Bao la Mkono’ – Video

MBUNGE wa Mtama na aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ametoa ufafanuzi kufuatia kauli yake aliyoitoa mtandaoni jana akisema “Nilaumuni kwa ‘bao la mkono’ sio hili la JF…” kauli iliyoibua mijadala mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.

 

Nape amesema hayo wakati akizungumza na Global TV Online leo Jumatano, Juni 13, 2018 jijini Dodoma na kusisitiza kwamba kuhusu JamiiForum kufunga huduma zake mitandaoni hahusiki lakini amekubali kuwa yeye ndiye muasisi wa Msamiati wa Bao la Mkono kwenye siasa za Tanzania, na hakutoa kauli kwa maana ambayo watu wamekuwa wakiizungumzia.

 

“Hili bao la mkono lilikuwepo kwenye shughuli nyingine hapa duniani, lakini kwenye misamiati ya siasa za pengine halikuwepo, nilipoanza ndipo likawepo, hivyo nilikiri kabisa na kusema kwamba kama kuna matatizo yalijitokeza kutokana na kauli hii ya bao la mkono basi wa kulaumiwa ni mimi kwa sababu nilianzisha mimi wala sikutumwa na chama changu,” amesema Nape.

VIDEO: MSIKIE NAPE AKIFUNGUKA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment