Exim Yafuturisha Wateja Wake Tanga
IKIWA ni muendelezo wa utaratibu wake wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja na wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Benki ya EximTanzania mwishoni mwa wiki iliandaa futari maalum kwa ajili ya wateja wake mkoani Tanga.
Hafla ya futari hiyo ilifanyika Hotel ya Tanga Beach Resort jijiji Tanga ikihudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh Hashimu Mgandilwa pamoja na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo Sheikh Juma Luwuchu.