The House of Favourite Newspapers

FA, JIDE KUWEKA HESHIMA JUKWAA MOJA

BAADA ya kutofautiana kwa takribani miaka mitano, wakongwe kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ wanatarajia kukutana jukwaa moja, Jumamosi hii (Machi 31) ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip, Oysterbay.

 

Akizungumza na Showbiz, Jide alisema shoo hiyo itakuwa ya kihistoria kwake na kuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia vibao watakavyoimba yeye na MwanaFA kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka zaidi ya mitano.

“Sina mengi ya kusema zaidi ya vitendo jukwaani. Nitapiga live band jimbo zangu karibu zote,” alisema Jide.

 

Miongoni mwa nyimbo zilizotamba ambazo wataimba kwa pamoja mwanaFA na Jide usiku huo ni Hawajui, Msiache Kuongea, Wanaume Kama Mabinti pamoja na Sikiliza.

ANDREW CARLOS.

Comments are closed.