Fabregas: Fundi Wa Asisti Anayeacha Alama England
KIUNGO mahiri wa Chelsea , Cesc Fabregas anatazamiwa kulihama soka la England na bila shaka huenda ndio ikawa ndio kimoja, lakini anaondoka akiwa ameacha alama ya kuwa miongoni mwa mastaa waliowahi kung’arisha ligi hiyo.
Fabregas, ambaye anataz a m i w a k u jiung a na M o n a c o y a Ufarans a , atakumb u k w a kwa sifa ya kama miongoni mwa mastaa wakali wa asisti.
Fabregas alianzia soka yake katika kituo cha kulelea yosso cha La Masia ambacho kinamilikiwa na Barcelona.
Akiwa na umri wa miaka 16 alichukuliwa na Arsenal na kujumuishwa katika timu yao ya yosso Septemba, 2003.
Kutokana na Arsenal kukabiliwa na tatizo la majeruhi, alipenya katika kikosi cha kwanza cha Arsenal msimu wa 2004/05.
Alivunja rekodi nyingi za klabu ya Arsenal na mwaka 2005 alitwaa taji la Kombe la FA,
Hata hivyo, kutokana na kuwa na ndoto ya kuchezea timu yake ya utotoni, aliondoka Agosti, 2011 na kurudi Barcelona kwa uhamisho uliogharimu kiasi cha pauni milioni 35.
Alidumu Barcelona kwa miaka mitatu, ambako Fabregas akishirikiana na mastaa wengine Lionel Messi, Xavi Hernandez na Andres Iniesta alitwaa taji la La Liga, the Copa del Rey, Klabu Bingwa ya Dunia, UEFA Super Cup na mataji mawili ya Spain Super Cup.
Alirudi England mwaka 2014 lakini ingawa hakurejea Arsenal badala yake alijiunga na Chelsea kwa ada ya pauni milioni 30, ambako katika msimu huo alisaidia timu hiyo kunyakua Kombe la Ligi na ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kwa upande wa timu ya taifa, Fabregas alianza kuchezea Hispania mwaka 2006.
Pia alikuwemo kwenye kikosi kilichocheza Kombe la Dunia mwaka 2006, Euro 2008, Kombe la Mabara la FIFA 2009, Kombe la Dunia mwaka 2010, Euro 2012, Kombe la Mabara 2013, Kombe l a Dunia 2014 na Euro 2016.
Alitoa mchango mkubwa kwa Hispania kutwaa mataji Ulaya katika miaka yaani 2008 na 2012 na mafanikio ya kutwaa Kombe la Dunia 2010, ambapo alitoa pasi kwa Andres Iniesta kufunga bao la ushindi kwenye mechi ya fainali.
Fabregas enzi zake akiwa kwenye kiwango alikuwa kivutio kumtazama kutokana na umahiri wake wa kupiga chenga, kutoa pasi na kufunga mabao.
Staa huyo alikuwa na kipaji binafsi lakini mafanikio yake ni matunda ya kunolewa na kituo cha kulelea yosso cha La Masia ambacho kinamilikiwa na klabu ya Barcelona.
Fabregas ana uwezo wa kucheza nafasi yoyote katika kiungo lakini pia anamudu kucheza kama straika.
Makali ya Fabregas yanathibitishwa kuwa ni staa namba mbili mwenye asisti nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu England akiwa ametoa 111 akiwa nyuma ya mastaa kama Ryan Giggs na kuwazidi nyota kama Frank Lampard, Dennis Bergkamp, Steven Gerrard na David Beckham.
Fabregas pia ana sifa nyingine ya kucheza kwa ari na pia haogopi na tabia hizo na alikuwa anazo tangu akiwa mdogo.
M a t h a l a n i aliwahi kuifungia Arsenal kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona mwaka 2010 wakati akiwa amevunjika mguu.
Pamoja na kuwa Fabregas alichezea timu ambazo zilikuwa na wachezaji mahiri lakini mara zote nyota yake iling’ara pia.
Ingawa kuna baadhi ya watu wamekuwa wanamponda kuwa eti alikuwa akipata msaada mkubwa na hasa alipokuwa kwenye timu za Barcelona, na Chelsea.
Hata hivyo, Fabregas alikuwa mkali kwani ukiangalia akiwa Arsenal alipewa unahodha akiwa na umri mdogo lakini pia aliiongoza timu hiyo ikiwa haina fungu kubwa la kusajili mastaa kutokana na kulipa deni la ujenzi la Uwanja wa Emirates.
Fabregas alikuwa anaiongoza Arsenal katika kipindi ambacho ilikuwa imewapoteza mastaa kama Thierry Henry, Patrick Vieira na wengineo, ambao ndio walikuwa chachu ya kikosi cha kutisha cha Arsenal kilichomaliza Ligi Kuu England bila ya kupoteza mechi msimu wa 2003/04.
LONDON, England.
Comments are closed.