The House of Favourite Newspapers

Fagio La Robertinho, Vilio Vitatawala Simba, Ahmed Ally Azungumza na Championi

0
Kocha wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

MABOSI wa Simba wamepanga kuitumia siku ya Jumatatu ijayo kwa ajili ya kutangaza mastaa wao ambao watapewa mkono wa kwaheri ambao wametajwa kutokuwepo kikosini hapo na kocha wa timu hiyo, Roberto Oliviera ‘Robertinho’.

Hadi sasa Simba wameshatangaza majina ya watu kadhaa ambao wameachwa kwenye kikosi hicho akiwemo winga Mghana Augustine Okrah na baadhi ya wataalam wa benchi la ufundi.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema, Jumatatu ijayo wataendelea kutoa majina ya wachezaji waliopendekezwa kuachwa ndani ya klabu hiyo jambo ambalo litazua vilio kwa mashabiki wake.

“Tayari Bodi yetu inaendelea kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao ripoti ya kocha wetu Robertinho imetaka waachane na klabu maana kuna wenye mikataba na waliomaliza, hivyo majina yote tutayatoa kuanzia Juamatatu ijayo.

“Ripoti ya kocha imetaja namba kubwa ya wachezaji wanaotakiwa kupewa mkono wa kwaheri na miongoni mwao kuna wale ambao ni lazima kujadiliana nao kutokana na mikataba yao maana hatutaki kesi yoyote baada ya zoezi hili kuisha,” alisema Ahmed.

Stori na Musa Mateja

BAADA ya SIMBA KUACHANA NAYE, VUNJABEI AVUNJA UKIMYA, AWAANDIKIA SIMBA WARAKA HUU MZITO…

Leave A Reply