The House of Favourite Newspapers

FAHAMU CHANZO CHA MAUMIVU YA SHINGO-2

Wiki iliyopita tuliianza mada hii inayohusu maumivu ya shingo, kwa hakika uliweza kujifunza na kuweza kujua chanzo cha maumivu hayo na leo tunakwenda kuhitimisha mada hii.

ENDELEA…

MAUMIVU yanaweza kuwa makali kiasi cha kuingilia mwenendo wa kawaida wa kila siku wa mtu aliyeathirika yaani mgonjwa wa shingo. Yako mambo ya msingi yanayoweza kufanyika nyumbani ili kumsaidia mtu kutatua tatizo hilo au kulipunguza makali mpaka  litakapoisha lenyewe.

HUDUMA YA KWANZA

Njia rahisi katika siku za awali kwa huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa shingo anaweza kuweka barafu sehemu inayouma kwa dakika 10-15, barafu iwekwe ndani ya katika mfuko wa kitambaa na unaweza kurudia kukanda sehemu hiyo inayouma kadiri ya uwepo wa maumivu. Baada ya hapo siku za zijazo unaweza kutumia na kukanda kwa maji ya moto kwa kutumia kitambaa, au mfuko maalum wa maji moto au kuoga maji ya moto.

Si mbaya kufanya usuguaji (masaji) taratibu au kuchua kwa kutumia mafuta maalum au kutumia dawa za maumivu za ute mzito za kuchua sehemu inayouma kwenye shingo. Mwisho unaweza kutumia dawa za kawaida za maumivu kwa ajili ya kukupa utulivu. Pata mapumziko ya kutosha na hakikisha unasitisha shughuli za kuchokoza maumivu haya.

USHAURI

Mgonjwa unashauriwa kuepuka kulalia mto mpaka upone, wakati unaumwa epuka matumizi ya vitu kama kompyuta au kama ni fundi cherehani, epuka kushona kwa muda kwani vitu hivyo vinachangia shingo kupinda wakati wakutumia na vilevile vitu vingine vitakavyosababisha kuinamisha shingo kama vile kuchona vitambaa, kusuka mkeka na kadhalika. Maumivu yakizidi muone mtaalamu wa afya ambaye anaweza kukupa dawa za kumaliza tatizo.

Mwisho.

Comments are closed.