The House of Favourite Newspapers

Fahamu Haya Kuhusu Televisheni za Ndani Kurusha Matangazo Bila Malipo ya King’amuzi

SERIKALI imesema jumla ya vituo 16 vya runinga vya ndani ya nchi, vikiwemo ITV, Channel 10, CloudsTV vimepewa leseni ya FTA (Free to Air) ambapo vituo hivyo vinapaswa kuwalipa warusha matangazo ili vionekane hata baada ya malipo ya king’amuzi kwisha.

Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema.

“Televisheni zote za ndani zilizo na leseni ya FTA (yaani Free to Air) zinapaswa kuonekana hata baada ya malipo kwisha. Kwa kanuni mpya mwenye kituo cha TV anapaswa kuwalipa wasafirisha masafa hayo ili wewe uone bure… asipolipa anaweza kukatiwa huduma.

“Suala la AzamTV kukata liko Baraza la Ushindani. Tusubiri uamuzi. Warusha matangazo wengine kama StarMedia na wengineo TV za ndani zinapaswa kuendelea kuonekana isipokuwa kama wamefutiwa huduma kwa kutomlipa mrusha masafa,” ameandika Abbasi kupitia Twitter.

Comments are closed.