The House of Favourite Newspapers

Shilole, Uchebe Mnaweza Kuushangaza Ulimwengu!

Msanii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (katikati) akiwa na mpenzi wake waliyefunga naye ndoa, Ashraf Uchebe (kushoto) katika picha ya pamoja baada ya ndoa hiyo jijini Dar es Salaam.

KWANZA kabisa nimshukuru Mungu kwa kuweza kusherehekea vyema Sikukuu ya Krismasi, bila shaka nawe mpenzi msomaji u miongoni mwao. Huku shauku kubwa ya leo ni kufungua zawadi.

 

Ikiwa bado hatujamaliza mwaka 2017 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2018, barua yangu ya leo, imfikie dada yangu Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye ni msanii wa Muziki wa Bongo Fleva aliyefunga pingu za maisha na mwandani wake, Ashraf Uchebe ‘Kibenten’ usiku wa Desemba 6, mwaka huu eneo la Masaki jijini Dar.

 

Ingawa ndoa yao haikuwa na mambo mengi sana kama inavyokuwa kwa mastaa wengine, lakini bado ilikuwa na figisufigisu za hapa na pale ikiwemo madai ya Shilole kuolewa na kijana mdogo anayemzidi sana umri ‘kibenten’.

 

Lakini jambo la kumshukuru Mungu dada yangu Shilole na ‘shemela’ Uchebe walimaliza vyema ndoa yao na sasa wanaendelea na maisha kama mume na mke. Ni jambo jema sana.

Mimi binafsi nawatakia maisha mema na yenye fanaka tele katika ndoa yao. Jambo ambalo nataka kumwambia Shilole na mumewe, kuwa watu wengi wanasubiri kuona kama Shilole atadumu na Uchebe kwenye hiyo ndoa kwa sababu wengi wanaamini kuwa dada ameolewa na kibenten ambacho hakitakuwa na uwezo wa kumkontroo hiyo anachokitaka yeye ndiyo hicho lazima kifanyike. Wengine wanaamini kuwa Shilole ni mtu wa ngumi mkononi mnapokorofishana.

 

Inawezekana dada yangu Shilole historia yako kwa wapenzi wako wa awali ikawa inakuhukumu na hata mambo yako ambayo umewahi kuyafanya ndiyo yakawa yanakutafuna.

 

Dada Shilole pamoja na yote ambayo umekuwa ukikutana nayo na pengine unayo, lakini bado unaweza kuushangaza ulimwengu kwa kuwa mwanandoa bora kabisa na mwenye kuigwa kama mfano na wasanii wenzako na jamii kwa ujumla.

 

Kama kweli mmeamua kuishi kama mume na mke basi, tabia na mambo yenu yaende kimke na mume. Achaneni na mambo ya kisela. Ni muda muafaka kwako Shilole kuwaaminisha watu kuwa unaweza kuwa mama bora na mwenye kuigwa na wasanii wenzako lakini na hata jamii nzima.

 

Kwa kuwa mmeamua kuoana na ninyi ndiyo ambao mliridhiana na kukubaliana kuishi kwa pamoja basi komaeni na ndoa yenu. Pambaneni na familia yenu. Kila mtu ana haki ya kuzungumza kile anachokifikiria akilini mwake lakini ninyi kama wana ndoa mna wajibu wa kutimiza majukumu yenu kama mwili mmoja.

Kama wewe ulivyo msanii una wajibu pia wa kuwahakikishia mashabiki wako kuwa wewe ni msanii wa kike na unaweza kuwa mama bora mwenye familia nzuri.

Bora Uchebe Afe Kuliko Kumkosa Shilole

Jamii kubwa inakuchukulia Shilole kama siyo mwanamke unayeweza kudumu kwenye ndoa na kuweza kuwa mama wa familia mwenye tabia ya kuigwa kutokana na baadhi ya makandokando yenye kutia shaka kuhusu maisha na tabia zako za kila siku.

 

Mengi yamesemwa na yatasema lakini kwa kuwa ninyi ndiyo mliopenda na mmeridhiana kuishi kama mke na mume basi endeleeni, pambaneni kushindana na maneno ya wafitini wenu.

 

Ushauri wangu kama kweli dada Shilole ulikuwa ni ngumi mkononi pindi unapokorofishana na waliotangulia basi jirekebishe. Kama kukitokea sintofahamu na mume wako jaribu kuzungumza naye kwa staha kwani amani haiji kwa kupigana bali kwa kuzungumza na kuridhiana.

 

Shilole wengine wanataka kuona kama uliachana na Nuh Mziwanda ambaye naye ilionekana ni kibenten kwako, waone kama utaweza kuishi na Uchebe.

Yote kwa yote Shilole kama kweli umeamua kuolewa na kuishi kama mke wa mtu basi unaweza, naamini kuna mambo ya ajabu ambayo yalikuwa yamezoeleka kwako yatapungua. Haitapendeza mke wa mtu kukuona ukiwa umevaa vi nguo vya ajabu, mara umefanya mambo ambayo yanastahili pengine kufanywa na watoto wa shule.

Mcheki Gigi Money Akijibebisha kwa Mpenzi Wake Usiku wa Krismasi

Comments are closed.