The House of Favourite Newspapers

FAHYMA ATAJA SIRI PENZI LAKE NA RAYVANNY KUDUMU

MZAZI mwenzake na msanii anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma ametaja siri inayomfanya kudumu na mpenzi wake huyo kwa muda mrefu.

 

Akipiga stori na Amani, Fahyma alisema kwamba, watu wengi huwa wanahisi yeye na mzazi mwenzake hawagombani kitu ambacho si kweli, huwa wanagombana mara nyingi ila upendo na uvumilivu ndivyo vinawafanya waendelee kudumu mpaka sasa.

 

“Kuna watu huwa wanafikiri mimi na mzazi mwenzangu hatugombani, kitu ambacho si kweli huwa tunagombana sana tu, ila sema binafsi nilishaamua kutulia naye, nampenda basi inatosha na ndiyo maana hamjawahi kusikia nina bwana mwingine zaidi yake,” alisema Fahyma.

Stori: Memorise Richard

Comments are closed.