The House of Favourite Newspapers

Fainali ya Shika Ndiga Yafana, Wawili Waondoka na Ndinga

0

Umati uliofurika kufuatilia fainali ya Shika Ndinga

Suleiman Mlela, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), akisoma majina ya washindi

Meneja Mkuu wa Efm, Denis Ssebo (mwenye mic) akizungumza jukwaani

Mshindi wa gari, Joyce Daniel akikabidhiwa hati ya ushindi.

Mshindi wa gari, Michael Peter akikabidhiwa hati ya ushindi.

Fainali ya Shindano la Shika Ndinga lililokuwa likiendeshwa na Kituo cha Redio cha Efm, hatimaye jana ilifikia mwisho katika ‘event’ kubwa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, huku Joyce Daniel na Michael Peter wakiibuka washindi wa jumla na kila mmoja kujinyakulia gari aina ya Toyota Carry (Kirikuu).

Katika event hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Suleiman Mlela, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wasanii Man Fongo, Sholo Mwamba, Virus na Chemical, walikinukisha kwa sana na kuzikonga nyoyo za mamia ya watu waliokuwa wamefurika kwenye viwanja hivyo.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Efm, Denis Ssebo, tangu kuanza kwa shindano hilo Machi 3, 2017, wamefanya matamasha kwenye jumla ya wilaya sita za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, zikiwemo Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala, Kibaha na Bagamoyo ambapo jumla ya washindi 14 walipatikana, 12 wakijinyakulia bodaboda na wawili wakijinyakulia magari.

“Lengo kuu lilikuwa ni kuhakikisha jamii inafaidika kupitia Efm radio na kuwawezesha kiuchumi. Tunaamini zawadi tulizowapa washindi wetu, zitawakomboa kiuchumi kwa kuanzisha biashara,” alisema Ssebo.

Leave A Reply