The House of Favourite Newspapers

Familia ya bilionea Msuya yataka usimamizi wa mirathi

0

msuyaNa JANETH MUSHI, ARUSHA

WAKATI mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Msuya akisota rumande kwa tuhuma za mauaji ya wifi yake, Aneth Msuya, wanafamilia ya bilionea huyo wamefungua kesi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi.

Baba wa marehemu Msuya, Elisaria Msuya pamoja na dada yake, Dk, Esther Msuya wamewasilisha maombi hayo kupitia shauri namba 3 la mwaka 2016.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Fatuma Masengi, wadai hao wanaiomba mahakama kuwateua kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo ambayo ni pamoja na nyumba aliyokuwa akiishi marehemu eneo la Kwa Idd, magari ya kifahari na shamba la hekari 109 lililopo eneo la Kisongo.

Mali nyingine ni pamoja na hisa za Kampuni za SG Nothern, Adventure Ltd, Unique Mining Company na Hoteli ya SG Resorts ambayo wakurugenzi wake ni mke wa marehemu na watoto wake. Mali zote zinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2.

Miriam na mwenzake, wanakabiliwa na mashitaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, Aneth.

Awali Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kupitia shauri namba 8 ya mwaka 2013 lililoamuliwa na Jaji Moshi, ilimteua Miriam kuwa msimamizi wa mali za mumewe.

Pamoja wazazi kupinga uteuzi wa Miriam, tayari watoto wawili wa bilionea Msuya wamefikisha umri unaokubalika kisheria kuwa wasimamizi wa mali za marehemu baba yao.

Leave A Reply