The House of Favourite Newspapers

FAMILIA YA MENINAH YALALA MBELE NA MWIJAKU!

WAKATI upelelezi wa kesi ya picha na video chafu za msanii wa filamu na muziki Bongo, Menina Attick ‘Meninah’ ukiendelea, familia yake imeapa kulala mbele na mtuhumiwa wao namba moja, Burton Mwemba ‘Mwijaku’.  Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, ndugu mmoja wa Meninah aliyejitambulisha kwa jina la Kessy Hassan amefunguka mengi kuhusu tukio hilo lililomkuta ndugu yao wiki mbili zilizopita. Kwa mujibu wa Kessy, video na picha chafu za Meninah zilizosambaa mitandaoni, ni jambo la aibu kwa wanawake wote. Hivyo kuiomba Serikali iendelee kufanya uchunguzi dhidi ya aliyehusika kusambaza na achukuliwe hatua kali.

Ndugu huyo ambaye naye anajishughulisha na muziki alisema, aliumia mno kuona video ya mwanamke mwenzake ikisambaa huku watu wakishadadia bila kujua kuwa mwenzao anaumia kiasi gani. “Huwezi kuamini, siku ya kwanza nilipoiona ile video nilishtuka sana kwa sababu Meninah ni ndugu yangu na mimi ni mdogo wake. “Huwa tunakaa na kuzungumza mambo mengi sana kuhusu kazi na maisha yetu kwa ujumla.

“Sasa ilipotokea ile ishu, nilisikitika sana kwamba ilikuwaje mpaka akashawishika kurekodi video akiwa faragha na kumtumia huyo mpenzi wake ambaye mwisho wa siku anaonesha wazi kuwa hakumpenda bali alitaka tu kumtumia kisha kumdhalilisha kama alivyofanya.

“Yaani huyo mtu amemtumia kisha akamdhalilisha, sasa hivi kila mwanaume anamjua Meninah jinsi alivyo. Anajua kabisa kwamba kumbe huyu msichana yupo hivi. “Jambo hili linatudhalilisha wanawake wote, siyo yeye tu. Kwa hiyo niliumia sana na bado anaendelea kuumia, lakini niseme tu kwamba huu mwaka hautaisha, lazima Mwijaku atalipa kwa alichokifanya.

“Yaani ikithibitika kuwa kweli yeye ndiye aliyehusika, atajutia kwa alichokifanya. Mimi amenikera sana kwa hiyo lazima alipie kwa alichokifanya,” alisema Kessy. Baada ya video na picha za Meninah kusambaa mitandaoni, kuna tetesi zilivuma kwamba mwanamama huyo alitoweka nyumbani anakoishi kwa siku tatu huku simu yake ikiwa haipatikani, lakini mdogo wake anajibu kamili.

“Unajua lile tukio lilikuwa ni la kwanza kumtokea Meninah, hivyo kwa hali ya kawaida, hata ungekuwa wewe, lazima ungefanya kama alichokifanya yeye. “Kitu kilichomjia kwa haraka akilini mwake ni kwenda mbali na watu, yaani kujitenga kwa muda ili asiendelee kusikia yale yaliyokuwa yanasemwa na walimwengu, ndiyo maana akafanya hivyo.

Comments are closed.