Familia ya Msaidizi wa Membe Yamwangukia JPM

FAMILIA ya msaidizi wa Bernard Membe, Allan Kiluvya,  anayedaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Julai 7, imeomba msaada baada ya kufanya jitihada za kumtafuta vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam bila mafanikio.

 

Ndugu hao wamejitokeza jana Julai 8, kuomba msaada kwa Rais  John Magufuli, serikali na Watanzania kwa ajili ya kufanikisha kumpata ndugu yao huyo.

 

Akizungumza kwa niaba ya familia, mjomba wa Allan, Samwel Ng’andu, amesema kutokana na jitihada walizozifanya lakini sasa wameshaanza kukata tamaa ya kumpata ndugu yao.

 

”Alikuwa kwenye matembezi ya jioni na dada zake, wakati anawarudisha nyumbani, alipowafikisha na kutaka kutoka, ile anageuza gari, ghafla ilitokea gari ikam-block (ikamkinga) kwa nyuma kiasi ambacho alishindwa kugeuza, na kwa sababu alikuwa amekunywa kidogo obviously (ni dhahiri) alikasirika kidogo, alishuka na kisha dereva wa lile gari jingine alishuka.,’ alisema Ng’andu.

 


Aliendelea:  ”Ghafla akawa amezungukwa na watu sita, na ndipo walipomvamia Allan, na akaanza kuomba msaada kwa dada yake Magreth ambapo alipoonyesha dalili ya kupiga kelele, mmoja wa watu hao alitoa bastola na kumwekea kichwani.

 

“Baada ya Magreth kuanza kupiga kelele ndipo ndugu wengine walipoamka na kukusanyana kwenda, kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Kawe majira ya saa nane usiku.”

 

Aidha, Ng’andu ametoa wito kwa viongozi mbalimbali wa dini, kuendelea kumuombea Allan ili kokote aliko awe kuwa salama.

 

Kwa mujibu wa wanafamilia, gari iliyomteka Allan ni Land Cruiser yenye namba za usajili T 810 BQS rangi ya kijivu na gurudumu lake limefunikwa na rangi ya chungwa.

 

WAZIRI Bashungwa AICHARUKIA NDC “Nataka majibu, wakulima wadogo tubadilishe maisha yao”


Loading...

Toa comment