The House of Favourite Newspapers

Familia ya Mshukiwa wa Mauaji ya Watoto 14 Yagoma Kuzika

0

FAMILIA ya mshukiwa sugu wa mauaji ya watoto zaidi ya 10, Masten Wanjala aliyekiri ambaye aliuliwa kwao baada ya kutoroka kutoka mahabusu ya polisi imemkana.
 
Familia ya Masten Wanjala imesema haitamzika kwa sababu inahofia kupata laana. Familia hiyo iliamua hata kukwepa kushiriki uchunguzi wa mwili wa mtoto wao kwa njia ya DNA uliofanywa na maafisa wa uchunguzi wa mwili kwa kuogopa laana.
 
Naibu Chifu wa Mukhweya Abiud Musungu alisema kuwa familia ya Wanjala ilikataa kupokea simu kutoka kwa maafisa ili wachukuliwe vipimo vya vinasaba-DNA na kumzika mtoto wao huyo wa kiume.
 
Masten Wanjala, aliyekuwa na umri wa miaka 20, alikutwa katika nyumba iliyopo katika mji wa Bungoma Magharibi mwa nchi hiyo, baada ya kutoroka mahabusu ya polisi Nairobi na kupigwa hadi kufa na wanakijiji wenye hasira.
 
Kabla ya kifo chake Hasten Wanjala alikiri binafsi kuwauwa watoto 10 katika kipindi cha miaka mitano. Pia alikiri kuwavuta na wakati mwingine hata kunywa damu yao.
 
Aliripotiwa kurudi katika nyumba ya wazazi wake ambao walikuwa tayari wamemkataa- na hatimaye alipigwa na kunyongwa na majirani ambao walibaini kuwa alikuwa pale, zilisema taarifa za vyombo vya habari nchini Kenya.
Leave A Reply