The House of Favourite Newspapers

Familia Ya Shabiki Wa Yanga Aliyefia Kwa Mkapa Waomba Msaada Serikali Na Yanga

0

Familia ya marehemu William Ernest aliyefariki katika Uwanja wa Mkapa alipokwenda kushuhudia mechi ya fainali ya kwanza ya Yanga dhidi ya USM Alger wanaomba msaada wa Serikali na Yanga ili kusafirisha mwili jijini Dodoma.
“Baba alikuwa anaipenda sana Yanga anaweza asifike nyumbani akaenda kuangalia mechi bila kuonana na sisi na hata mechi ya jana alikuwa amekuja akitokea Morogoro na aliondoka nyumbani asubuhi,” alisema Dorrah mtoto wa marehemu William.
Pia amesema taarifa za msiba walizipata saa 1 usiku kutoka kwa Dk Kimaro akiwataka waende kumuona William kwani anaumwa na alipata majeraha sehemu ya kichwani kutokana na mkanyagano.
Naye shemeji wa marehemu Grace Lucas amesema wamepata pigo sababu marehemu ndiye tegemeo la familia na ana watoto wanaosoma.
“Mke hana kazi na hapa tulipo wamepanga hivyo hatuna chakula na mchana majirani walitusaidia ila jioni yetu hatuijui,” amesema Grace.
William alikuwa anajishughulisha na uuzaji wa nyama Morogoro na Dodoma na ameacha mke na watoto wanne ambao wawili wanasoma shule ya msingi.

YANGA: TULIENI HAWA TUTAWATOA KWAO/ STRAIKA MKONGO APIGA MKWARA MZITO SIMBA SC | KROSI DONGO

Leave A Reply