The House of Favourite Newspapers

Familia yamzuia Rose Muhando kwenda kanisani!

1

rose_muhandoKATAZO! Nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando (pichani) amezuiwa kuingia kanisani na ndugu zake wa damu kufuatia kile walichokiita ni kuchoshwa na manyanyaso na kwamba endapo akienda kinyume na maagizo hayo watachukua walichokitaja kuwa ni uamuzi mgumu, Amani linatumbua jipu!

Kwa mujibu wa chanzo makini, siku nyingi nduguze wamekuwa wakimtaka Rose kuachana na Ukristo, lakini amekuwa ‘ngangali’ kwa kuwa anafurahia huduma anayoitoa.

Hata hivyo, Rose anadaiwa kuwa na msimamo wa kutokubaliana na ndugu hao lakini hivi karibuni alinyoosha mikono kwa kutii amri kwamba, ndugu zake hawataki wamuone akiingia kanisani.

“Kulikuwa na kikao kizito sana. Rose alitakiwa afanye uamuzi mgumu kwani maneno makali ambayo amekuwa akizushiwa kwamba tapeli, mara anabwia unga, si tu kwamba yanamuumiza peke yake, hata ndugu hao. Ndiyo maana wameamua kumzuia kwa nguvu zao zote kwenda kanisani,” kilisema chanzo kimoja.

Juzi, paparazi wetu alimtafuta staa huyo kwa njia ya simu ili kujiridhisha kwa kina na madai hayo ambapo kwa sauti ya juu, alisema:

“Jamani! Unajua mimi naumwa! Nadhani tuliwasiliana siku za nyuma (anamkumbusha mwandishi). Kwa hiyo tangu siku zile bado hali yangu kiafya haijakaa sawa na ndiyo maana sijaenda kanisani.

“Ni kweli kuna msuguano wa aina hiyo na ndugu zangu. Si unajua hawajawahi kupendezwa na uamuzi wangu wa kuhama Uislamu. Lakini mara zote nimekuwa nikiwaambia hakuna wa kuniondoa kwenye Ukristo maana najua huyu Yesu alikonitoa.

“Kuna kaka yangu huyo ndiyo amekomaa kunikataza. Nilimwambia mchungaji wangu (hakumtaja jina), akamfuata lakini kaka akampiga mkwara mzito, yaani we acha tu.”

1 Comment
  1. Edward kiboko says

    Imani nikokote dada rose muamini mungu ipo siku yataisha na vile vile penye uzuri lazima vikwazo vitokee

Leave A Reply