The House of Favourite Newspapers

Faru Mweusi Afariki Akisafirishwa Kutoka Uingereza Kuja Tanzania

FARU dume aliyekuwa akisafirishwa kutoka hifadhi ya Port Lympne nchini Uingereza amefariki akiwa kwenye ndege wakati akisafirishwa kuja Tanzania.

 

Taasisi ya Aspinall inayosimamia hifadhi ya Port Lympne imesema kuwa hadi sasa haijafahamika chanzo cha kifo cha faru huyo lakini imesema watafanya uchunguzi wa haraka.

 

Faru huyo aliyepewa jina la Zambezi alikuwa akisafirishwa kwa ushirikiano wa mradi wa Grumeti na Serikali ya Tanzania kama sehemu ya makakati wa kuongeza idadi ya faru weusi kwenye Hifadhi ya Serengeti.

 

Comments are closed.