Polisi Waua ‘Majambazi’ Sugu, Mambosasa Amfungukia Msaidizi wa Zitto – Video

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwauwa liliodai ni majambazi sugu wawili na kukamata silaha mbili ndogo zikiwa na jumla ya risasi tano.

 

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Julai 4, 2019, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, SACP Lazaro Mambosasa, wakati akizungumza na wanahabari aliposema tukio hilo lilitokea  Julai 1, mwaka huu katika maeneo ya Kitunda, jeshi hilo lilipopambana na majambazi hao na kufanikiwa kuwadhibiti.

 

,Aidha, jeshi hilo limewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuwabaini wahalifu kabla hawajasababisha madhara.

 

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limetoa taarifa ya kupatikana kwa msaidizi wa Zitto Kambwe ambapo amepatikana Mombasa nchini Kenya.

MSIKIE MAMBOSASA AKIZUNGUMZA HAPA


Loading...

Toa comment