The House of Favourite Newspapers

Fastjet yasherehekea miaka sita ya kutoa huduma zake hapa Nchini

KATIKA kusherehekea mika sita ya Shirika  la ndege la Fastjet hapa nchini pia  linadhamini usafiri wa ndege  kwa Chama cha watoa huduma ya kinywa na meno Tanzania (TDA) na  zaidi ya madaktari 20 pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu kwa ajili ya kutoa huduma ya afya ya meno kwa mamia ya watu Mjini Butiama wakati wa kongamano la 33 la wanasayansi wa huduma za afya ya meno.

 

 

‘Kama sehemu ya utowaji wa huduma kwa jamii, Fastjet inafuraha kubwa kuweza kutoa marejesho kwa jamii wakati tukisheherekea miaka 6 ya utoaji wa huduma ya anga Tanzania’.

 

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet Lawrence Masha ambaye pia alisema” Ni heshima kubwa kuweza kubadilisha maisha ya watoto na jamii kwa ujumla kwa kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa madaktari ambao ni watalaam kutoka hospitali ya Muhimbili iliopo Dar es salaam kwenda Mwanza kutoa huduma ya afya ya meno kwa watoto pamoja na watu wengine ambao hawawezi gharama ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa matibabu.’

 

 

‘Fastjet inaendelea kutimiza ahadi yake kwa Wateja kwa kutoa huduma bora zaidi kwa gharama nafuu. ‘Hivi karibuni tulizindua huduma mpya ambayo Wateja wote wanaosafari na fastjet wanapata viburudisho bure kwenye ndege zetu pamoja na uzito wa kilo 23 ya mizigo unaoingizwa ndani na kilo 23 ya mzigo unaobebwa mkononi’. Aliongezea Ndugu Masha.

 

 

‘Tumeweza kufikia wastani asilimia 90 ya malengo ya muda Tanzania katika mwaka wa 2018 natunavyo sherekea miaka 6 ya fastjet Tanzania lengo letu nikutoa huduma kwa wakati ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuboresha huduma kwa Wateja kwa ujumla.’

 

 

Fastjet inaruka kati ya Dar es salaam na Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Lusaka na Harare na ndege zenya ingini za jet.

Kuhusu Fastjet:

Fastjet ni shirika lenye tuzo mbalimbali (Kama Skytrax World Airline Awards Best Low-Cost Airline in Africa 2017 na Leading African Low-Cost Carrier, World Travel Awards 2016 and 2017 ) Shirika hili lililoanza shughuli zake Tanzania mwaka 2012, kwa kusafirisha abiria kati ya Dar es salaam na Kilimanjaro na Mwanza pekee. Leo, Fastjet inasafirisha abiria ndani ya Tanzania kati ya Dar es salaam na Mbeya, Kilimanjaro na Mwanza huku ikiwa na safari za kimataifa kutoka Tanzania kwenda Harare, Zimbabwe na Lusaka, Zambia.

 

Fastjet ilianza safari za ndani ya nchi ya Msumbiji kati ya Maputo na Beira, Nampula na Tete Tarehe 3 Novemba 2017 na pia ilisherehekea mwaka wake wa pili wa kufanya shughuli zake ndani ya Zimbabwe mwaka jana. Shirika lnafanya shughuli zake kati ya Harare na Victoria Falls, Harare Dar es Salaam na Kutoka Harare na Victoria falls kwenda Johanesburg, South Africa.

 

Shirika hili tayari limeshasafirisha zaidi ya abiria Milioni 3, huku likiwa na rekodi nzuri ya kutua na kuondoka kwa wakati na kujijengea sifa ya kuwa shirika la ndege la kuaminika na nafuu.

Kwa taarifa zaidi:

[email protected]

Tel: 0713 843975

Comments are closed.